IQNA

Kituo kipya cha kuchapisha Qur'ani nchini Kuwait

11:32 - February 26, 2020
Habari ID: 3472506
TEHRAN (IQNA) – Kituo kipya cha kuchapisha Qur'ani Tukufu kitafunguliwa katika wilaya ya Sabhan mkoani Mubarak al-Kabeer.

Akitoa tangazo hilo, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Kuchapisha Qur'ani na Sunnah Kuwait Fahd al-Daihani amesema mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano na Wizara ya Masuala ya Kijamii na Leba nchini humo.

Aidha amesema bajeti kwa ajili ya mradi huo itakabidhiwa Wizara ya Biashara, Baraza la Mawaziri na Bunge kwa ajili ya kuidhibishwa.

Bajeshi ya kituo hicho imekadiriwa kuwa ni Dinari za Kuwait Milioni 12 na kinatazamiwa kuwa na uwezo wa kuchapisha nakala milioni tano za Qur'ani kwa mwaka.

3881043

captcha