IQNA

Kongamano la Kimataifa la Qur'ani kufanyika Uingereza

16:36 - March 29, 2017
Habari ID: 3470912
TEHRAN (IQNA)-Mji wa Oxford nchini Uingereza utakuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa la Qur'ani Tukufu baadaye mwaka huu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo litafanyika Julai 4 na limeandaliwa na Taasisi ya Qur'ani ya Chuo Kikuu cha Oxford.

Tovuti ya taasisi hiyo imedokeza kuwa, washiriki watajadili maudhui kadhaa zinazohusu utafiti wa Qur'ani Tukufu.

Kati ya mada za kongamano hilo ni pamoja na, kuibuka serikali za Kiislamu na miongozo ya Qur'ani zinazoifuata, sheria za Qur'ani na zinavyohusiana na sheria za kisekula na sheria za kimataifa, misingi ya Qur'ani katika mifumo ya Kiislamu ya kifedha na kibenki n.k.

Mkutano huo pia utajadili majibu ya Qur'ani kwa changamoto za kielimu na kifilosofia ambazo Waislamu wanakabiliana nazo, misingi ya Qur'ani katika harakati za kiroho na kisufi miongoni mwa Waislamu na namna vyombo vya habari vinavyoakisi maudhui za Qur'ani. Washiriki pia wataangaziambinu mpya za kufasiri Qur'ani Tukufu na taathira za masomo ya Qur'ani katika fikra za kidini kote duniani.

Waandalizi wa Kongamano la kimataifa la Qur'ani Tukufu wanasema linalenga kuwaleta pamoja wasomi na wataalamu wa Qur'ani ili kuwawezesha kubadilishana mawazo na kustawisha ufahamu wa Qur'ani..../  3470912

captcha