Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Abubakr Kanaan mkurugenzi mkuu wa Waqfu
wa Ahul Sunna katika mkoa wa Nineveh kaskazini mwa Iraq amesema tokea mwezi
Juni mwaka 2014 wakati magaidi wa ISIS walipoukalia kwa mabavu mji wa Mosul hadi
sasa, wembomoa misikiti 104.
Ameongeza kuwa mioni mwa misikiti hiyo 37 imebomolewa na magaidi hao wa
Kiwahhabi kutokana na kuwepo makaburi ndani yake. Halikadhalika afisa huyo wa
Waqfu amesema misikiti mingine 67 imebaribiwa kwa mabomu na magaidi wa ISIS na
aghalabu haiwezi tumika tena kutokana na uharibifu mkubwa na hivyo inapaswa
kujengwa upya.
Kanaan amesema magaidi wa ISIS wameharibu maeneo mengi ya kihistoria na
turathi muhimu za Kiislamu mjini Mosul, mji wenye historia ndefu.
Magaidi wa Kiwahabbi wa ISIS waliianzisha kampeni ya ukatili nchini Iraq
mnamo Juni 2014 wakati walipouvamia na kuuteka mji wa Mosul. Magaidi hao
wametekeleza jinai za kinyama dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni,
Shia na pia Wakristo katika maeneo waliyoyateka
Iraq. Serikali ya Iraq inasema baadhi ya nchi jirani kuwa ndizo zinazounga
mkono kundi la ISIS.