IQNA

55 wauawa katika hujuma za kigaidi misikitini Nigeria

14:51 - October 25, 2015
Habari ID: 3393551
Hujuma mbili za kigaidi zilizolenga misikiti kaskazini mashariki mwa Nigeria zimepelekea watu wasiopungua 55 waliuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Ijumaa watu 27 walipoteza maisha wakati magaidi walipofanya shambulio kwenye msikiti mpya wa Jambutu Juma’at katika mji wa Yola jimboni Adamawa. Hujuma hiyo ilijiri wakati waumini wakiendelea na Sala ya Ijumaa. Aidha Ijumaa alfajiri watu wengine 28 waliuawa baada ya gaidi kujilipua katika msikiti wakati wa Sala ya Alfajiri mjini Maiduguri katika jimbo la Borno ambalo ni ngome ya magaidi wakufurishaji wa Boko Haram. Hakuna aliyedai kuhusika na hujuma hizo mbili lakini serikali ya Nigeria inaamini kuwa magaidi wa Boko Haram ndio waliotekeleza hujuma hizo dhidi ya misikiti.
Wakati huo huo Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bi. Marzieh Afkham amelaani hujuma hiyo huku akisisitiza umuhimu wa kuwepo jitihada za pande zote kukabiliana na misimamo mikali ya kidini.
Aidha Afkham amesema Iran iko tayari kubadilishana uzoefu wake na Nigeria katika vita dhidi ya ugaidi. Halikadhalika amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatoa mkono wa pole kwa serikali na watu wa Nigeria pamoja na familia za waliopoteza maisha au kujeruhiwa katika hujuma hizo za kigaidi.../mh

3393040

captcha