IQNA

Mufti wa Misri alaani Israel kwa kumuua mtoto Mpalestina

19:07 - August 02, 2015
Habari ID: 3338079
Mufti Mkuu wa Misri amelaani vikali kitendo walowezi Waisraeli kumuua kinyama mtoto mdogo wa Palestina siku ya Ijumaa.

Sheikh Shawqi Allam pia ameikosoa jamii ya kimataifa kwa kutochukua hatua yoyote ya maana kuhusu jinai hiyo ya Wazayuni hao wenye misimamo mikali. Ametoa wito kwa nchi za Kiarabu na Kiislamu pamoja na taasisi za kimataifa kuchukua hatua za kivitendo kuzuia unyama na ukatili wa Wazayuni dhidi ya Wapalestina wanaodhulumiwa.
Mapema Ijumaa walowezi wa Kiyahudi walishambulia kijiji cha Duma katika Ukingo wa Magharibi huko Palestina na kuchoma moto nyumba mbili za Wapalestina. Katika shambulizi hiyo la kinyama Wazayuni hao wamemchoma moto na kumuua mtoto mdogo aliyekuwa na umri wa miezi 18 kwa jina Ali Saad Dawabsha na kuwajeruhi vibaya wazazi na ndugu yake mwenye umri wa miaka minne.
Masetla hao Waisraeli wanaendelea kulaaniwa kimataifa kutokana na jinai yao hiyo ambayo imeweka wazi utambulisho wa kigaidi wa utawala haramu wa Israel.../mh

3337687

Kishikizo: wazayuni kiislamu shawqi
captcha