IQNA

Palestina kukabiliana na hujuma ya Wazayuni katika Msikiti wa Al Aqsa

11:06 - October 20, 2014
Habari ID: 1461999
Mahmoud Abbas Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameahidi kuchukua hatua za kisheria kuzuia walowezi wa Kizayuni kuuvuamia Msikiti wa Al Aqsa katika Baitul Muqaddas.

Akizungumza Jumamosi, Abbas alisema serikali ya Palestina haitawaruhusu walowezi wa Kizayuni waendelee kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa.  Ameongeza kuwa serikali ya Palestina itachukua hatua za kisheria katika uga wa kimataifa ili kuhakikisha kuwa walowezi wa Kizayuni hawauvamii Msikiti wa Al Aqsa.
Kauli hiyo ya Abbas imekuja baada ya Jumuiya ya Kizayuni ya wanafunzi wanaounga mkono 'Hekalu la Suleiman' kuvamia sehemu ya Msikiti wa Al  Aqsa katika uchokozi ambao umeibua hasira kali za Waislamu hasa wa Palestina. Wazayuni wenye kufurutu mipaka wakiwa chini ya himaya ya wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamewazuia Wapalestina kuswali ndani ya msikiti huo.
Katika wiki za hivi karibuni msikiti wa  kihisotoria wa Al Aqsa  umekuwa medani ya mapigano na ghasia baina ya Waislamu Wapalestina wanaotaka kuswali hapo ndani na walowezi wa Kizayuni. Katika kipindi cha siku 10 zilizopita, walowezi wa Kizayuni wasiopungua 1,300 wakiungwa mkono na mamia ya wanajeshi na polisi wa utawala haramu wa Israel wamekuwa wakiingia katika uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa. Haya yanajiri katika hali ambayo vikosi vya polisi wa utawala ghasbu wa Israel wanawazuia Wapalestina walio chini ya umri wa miaka 50 kuingia katika eneo hilo takatifu.
Huku hayo yakijiri, Khaled Meshaal, Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina Hamas ameonya kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia mwanya uliojitokeza kufuatia mgogoro katika eneo la Mashariki ya Kati ili kuudhibiti Msikiti wa Al Aqsa.
Ikumbukwe kuwa Msikiti wa Al Aqsa uko katika mji wa Quds au Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel. Eneo hilo ni takatifu na linaheshimiwa na wafuasi wa dini zote za mbinguni.
Lengo la njama za utawala wa Kizayuni katika Quds Shariff au Quds Tukufu ni kuuharibu na kuubomoa Msikiti wa Al Aqsa na mahala pake kujenga hekalu la Kiyahudi. Ni kwa msingi huo ndio katika miezi ya hivi karibuni tukashuhudia kuongezeka harakati za Kuuyahudisha Msikiti wa Al Aqsa ili hatimaye kuhakikisha kuwa ni Mayahudi tu wanaoruhusiwa kuingia katika msikiti huo mtakatifu. Mji wa Quds ulikaliwa kwa mabavu na Israel mwaka 1967. Mji huo mtukufu una maeneo ya kale na ya kihistoria ya Wapalestina na Msikiti wa Al Aqsa ni moja ya sehemu hizo ambazo sasa zinakabiliwa na hatari ya kuagamiza kutokana na hujuma za Wazayuni wenye misimamo mikali. Kwa maelezo hayo tunafikia natija kuwa kutokana na kushindwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya utawala wa Kizayuni kufuatia jinai zake za kivita huko Ghaza na kuharibu turathi za kitaifa na kidini huko Quds Tukufu ni moja ya sababu kuu ambazo zimepelekea utawala wa Kizayuni  upate kiburi cha kuwahimiza Wazayuni wenye misimamo mikali wauvamie na kuuharibu Msikiti wa Al Aqsa.../mh

1461648

captcha