IQNA

Kiongozi Muadhamu

Mapambano ya silaha,njia pekee ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni

22:14 - July 25, 2014
Habari ID: 1433169
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba, njia pekee ya kukabiliana na utawala wa kinyama wa Israel, ni kuwepo muqawama wa kutumia silaha wa Wapalestina na kupanuka wigo huo wa mapambano hadi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Ayatullahil Udhma Ali Khamenei aliyasema hayo Jumatano jioni mjini Tehran wakati alipokutana na wanachuo wa vyuo vikuu na vituo vya elimu ya juu hapa nchini. Kiongozi Muadhamu alielezea kadhia ya Ukanda wa Ghaza na kubainisha kuwa, jinai hizo zisizo na kifani, ni kielelezo cha dhati na hakika ya utawala huo wenye sifa za mbwa mwitu na unaoua watoto wadogo, na bila shaka dawa yake ni kuangamizwa na kutokomezwa kikamilifu utawala huo ghasibu. Ayatullah Khamenei amesema kuwa, masaibu yanayowakumba watu waliodhulumiwa wa Ghaza ni mfano wa sera za ukatili wa wazi na za ngumi ya chuma zinazotekelezwa kwa kiburi na utawala wa haramu na bandia wa Israel katika kipindi chote cha umri wake wa miaka sitini na sita. Jeshi la utawala wa Israel kwa kupata uungaji mkono wa Marekani kuanzia tarehe 8 Julai mwaka huu kwa mara nyingine tena ulianza kutekeleza mashambulio ya makombora katika eneo la Ghaza linalokabiliwa na mzingiro wa kidhulma kwa miaka kadhaa sasa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa masaibu yanayowasibu watu wanaodhulumiwa wa Ghaza ni mfano wa siasa za ukatili wa wazi na za ngumi ya chumi zinazotekelezwa kwa kiburi na utawala haramu na bandia wa Israel katika kipindi chote cha umri wake wa miaka 66.
Ayatullah Khamenei ameashiria matamshi ya mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Ruhullah Khomeini aliyesema kuwa "Israel inapaswa kufutwa kabisa" na kusisitiza kuwa: Kufutwa Israel hakuna maana ya kuangamizwa Wayahudi katika eneo hili bali suala hilo lina mantiki na utekelezaji wake wa kivitendo uliopendekezwa na Jamhuri ya Kiislamu katika duru za kimataifa.
Amesema kwa mujibu wa mantiki hiyo watu wanaoishi katika eneo hilo wanapaswa kushiriki katika kura ya maoani ya kuainisha serikali waitakayo na kwa njia hiyo utawala ghasibu na bandia wa Israel utatoweka.
Ayatullah Khamenei ameyahimiza mataifa yote ya Waislamu ya wasio Waislamu kuwaunga mkono kisiasa watu wa Ukanda wa Ghaza na kusema kuwa katika Siku ya Kimataifa ya Quds dunia itaona maandamano makubwa ya taifa la Iran. Amekosoa vikali misaada na uungaji mkono wa kuaibisha wa madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani kwa maafa makubwa yanayoendelea kufanywa na Israel na kusema kuwa nchi kadhaa za Magharibi hususan Marekani na Uingereza khabithi zinaunga mkono waziwazi jinai ambazo hazikubakliwi hata na mwanadamu wa kawaida, na Rais wa Marekani anajitokeza kwa maneno ya kejeli akisema kuwa Israel ina haki ya kujiulinda! Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa mwenendo huo wa nchi za kibeberu na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wa Ghaza vinaonesha kuwa nchi hizo haziamini haki za binadamu wala ubinadamu na maneno yote zinazoyasema kuhusu uhuru na haki za binadamu ni kuchezea shere uhuru na haki za binadamu.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa mtazamo unaoipinga Marekani na Magharibi nchini Iran ni mtazamo wa kimantiki unaotegemea tajiriba na mahesabu sahihi.

1432797

captcha