IQNA

Kaaba Tukufu

Pazia la al-Kaaba (Kiswa) labadilishwa mkesha wa Muharram

14:49 - July 19, 2023
Habari ID: 3477304
MAKKA (IQNA) – Kifuniko, kinachojulikana kama Kiswa, cha Kaaba Tukufu kilibadilishwa Jumanne usiku kwa mujibu wa desturi ya kila mwaka.

Kaaba katika Msikiti Mkuu wa Makka ilipokea pazia jipya linalojulikana kama Kiswa, kuashiria kuanza kwa Mwaka Mpya wa Kiislamu Jumatano, Julai 19.
Kaaba ndio sehemu takatifu zaidi katika Uislamu na Waislamu kote ulimwenguni huelekea katika eneo hili wakati wa Sala ya Ijumaa. Kwa kawaida Kiswa hubadilishwa kila mwaka siku ya tisa au 10 ya Dhu Al Hijja, mwezi wa mwisho wa kalenda ya Kiislamu, ambayo inaambatana na ibada ya Hija. Hata hivyo, mwaka jana, uamuzi wa kifalme ulihamisha tarehe hiyo hadi siku ya kwanza ya Muharram, mwezi wa kwanza wa kalenda ya Kiislamu.
Mchakato wa kubadilisha Kiswa unahusisha timu ya wataalamu ambayo huondoa kwa uangalifu kifuniko cha zamani na badala yake na mpya, upande kwa upande.

Kiswa ni pazia nyeusi ambayo hushonwa kwa hariri yenye uzito wa kilo 670 ambapo aya za Qur'ani hushonwa kwa uzi wa dhahabu katika pazio hilo.  Aya hizo hushindwa kwa dhahabu yenye uzito wa kilo 120 na uzi wa fedha wenye uzito wa kilo 100. Pazia ambalo huondolewa kukatwa vipande vipande na kutumwa katika nchi mbali mbali za Kiislamu kama zawadi kutoka kwa wakuu wa Saudia.

Kishikizo: muharram kiswa
captcha