IQNA

Pazia la al-Kaaba (kiswa) labadilishwa kabla ya Idul Adha

21:19 - August 20, 2018
Habari ID: 3471640
TEHRAN (IQNA)- Sherehe imefanyika mjini Makka Jumapili kubadilisha pazia la al-Kaaba Tukufu linalojulikana kama Kiswa.

Sherehe hiyo ilianza kwa mlango wa al-Kaaba kufunikwa kwa pazia hiyo ambalo baadhi ya sehemu zake zimenakishiwa  kwa uzi wa dhahabu.  Sehemu nne za pazia hilo zimepambwa kwa Surat al Ikhlas na aya nyinginezo za Qur'ani Tukufu.

Kila mwaka pazia la hariri ambalo huwa limefunika al-Kaaba hubadilishwa na jipya kuwekwa katika siku ya 9 ya Dhul Hija.

Pazia ambalo hutolewa hukatwa vipande vipande na kuzawadiwa wageni maalumu kutoka nchi za kigeni.

Pazia al-Kaaba (kiswa) labadilishwa kabla ya Idul Adha

Pazia al-Kaaba (kiswa) labadilishwa kabla ya Idul Adha

Pazia al-Kaaba (kiswa) labadilishwa kabla ya Idul Adha

Pazia al-Kaaba (kiswa) labadilishwa kabla ya Idul Adha

3739966

captcha