IQNA

Fiqhi Katika Qur’ani Tukufu: Juhudi za Kutumia Uwezo wa Qur'ani katika Fiqhi

20:56 - October 09, 2023
Habari ID: 3477704
TEHRAN (IQNA) – Fiqh katika Qur’ani ni kazi ya kufasiri Qur’ani Tukufu ambayo mwandishi ametafsiri Ayat al-Ahkam ya Kitabu kitukufu.

Ayatu al-Ahkamu ni aya za Qur'ani ambazo hukmu za kivitendo za Sheria au hukumu za kifiqhi zinaweza kutolewa.

Fiqhi katika Qur’ani ni kitabu cha Allameh Qutbuddin Ravandi, mwanazuoni mkuu wa Kishia wa karne ya 6 Hijria, Ni katika fani ya Fiqh (sheria) ya aya za Qur’ani Tukufu, zilizoandikwa kwa Kiarabu katika juzuu mbili,  Aliiandika kwa kuzingatia sura za vitabu vya fiqhi kuanzia Twahara (usafi) hadi Diya fidia ya pesa kwa familia ya mwathirika ambapo kifo kimetokea ama kwa kukusudia au kwa bahati mbaya.

Maisha ya Allameh Qutbuddin Ravandi

Qutbuddin Saeed ibn Abdullah ibn Hussein ibn Habatallah Ravandi Kashani, anayejulikana kama Qutb Ravandi, alikuwa mwanazuoni mkubwa wa Hadithi za Shia, mtafsiri wa Qur’ani Tukufu, mwanatheolojia, mwanasheria, mwanafalsafa na mwanahistoria wa karne ya 6 Hijria.

Alikuwa mwanafunzi wa Sheikh Tabarsi, mwandishi wa Majma al-Bayan Qur’ani Exegesis.

Qutb Ravandi aliandika vitabu vingi katika nyanja mbalimbali, miongoni mwa vile maarufu zaidi ni Al-Khara’ij wal-Jara’ih.

Alinufaika na elimu ya baba yake na pia kazi na mawazo ya watu wakubwa kama Sheikh Saduq, Sayyid Murtadha, Sayyid Radhi, na Sheikh Tusi.

Ufafanuzi Unaojadili Siri za Maneno na za Kiroho za Qu’rani Tukufu

Kwa mujibu wa kitabu Riyadh al-Ulama, Qutb Ravandi amesikia na kunukuu kutoka kwa wanachuoni wakubwa wa Hadithi wa Isfahan, Khorasan na Hamadan, jambo ambalo ni dalili kwamba alifanya safari nyingi kwa malengo ya kielimu.

Qutb Ravandi alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri walioonyesha ujuzi na umahiri katika nyanja mbalimbali za sayansi ya Kiislamu.

Alizikwa kwenye ua wa kaburi tukufu la Hazrati Masoumeh (SA) huko Qomu.

Msukumo wa Kuandika Tafsiri Za Qur’ani Tukufu

Mwandishi anasema katika utangulizi kwamba kilichomsukuma kuandika kazi hiyo ni kwamba hakupata kitabu chochote kilichoandikwa juu ya suala hili, ambacho kinasoma Fiqhi ndani ya Qu’rani na maneno ya Mwenyezi Mungu.

Ndio maana alianza kuchunguza masuala yote ya kifiqhi katika maneno, maana, sura na kina cha aya za Qura’ni zinazohusu hukumu za kivitendo za kisheria.

Vipengele vya Tafsiri Qur’ani Tukufu

Yaliyomo katika kitabu hiki yameandikwa kwa ufupi sana, Yaliandikwa kwa mpangilio wa masuala ya kifiqhi na inajumuisha mada zote mbili za tafsiri na fiqhi, Mwandishi ameathiriwa na maoni ya Sheikh Tusi na Sayyid Murtadha, lakini pia anatoa uchambuzi madhubuti wa kifiqhi na tafsiri  yake yeye mwenyewe.

Sifa nyingine ya kitabu hiki ni kwamba mwandishi anafaulu kufananisha maoni ya kifiqhi na tafsiri ya Qur’ani Tukufu ambayo yanaonekana kupingana.

 

3485485

 

 

captcha