IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 7 ya Qur'ani ya Kimataifa kwa Wanawake yanaendelea Dubai

19:57 - September 16, 2023
Habari ID: 3477607
DUBAI (IQNA) – Toleo la 7 la mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Sheikha Fatima Bint Mubarak kwa wanawake yalizinduliwa huko Dubai, katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), siku ya Jumamosi.

Sherehe za ufunguzi zilihudhuriwa na maafisa kadhaa, akiwemo Ibrahim Bu Milha, mshauri wa Mtawala wa Dubai kwa Masuala ya Utamaduni na Kibinadamu na mwenyekiti wa Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA).

Wahifadhi Qur'ani kutoka nchi 60 wanashiriki katika toleo la mwaka huu, ambalo litaendelea hadi Ijumaa, Septemba 22.

Mashindano hayo hufanyika katika vipindi viwili vya asubuhi na alasiri kila siku.

Siku ya Jumamosi, wawakilishi wa Misri, Bahrain, Malaysia, Austria na Singapore walijibu maswali ya jopo la majaji.

Jopo hilo linajumuisha wataalamu wa Qur'ani kutoka nchi mwenyeji pamoja na Misri, Oman, Bahrain, Saudi Arabia na Syria. Wajumbe wake watatu ni wataalamu wa Qur'ani wanawake.

DIHQA kila mwaka huandaa hafla ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanawake kutoka nchi mbalimbali.

4169236

Habari zinazohusiana
captcha