IQNA

Elimu

Mtafiti apongeza kazi zenye thamani za marehemu Wilferd Madelung

7:27 - May 13, 2023
Habari ID: 3476993
TEHRAN (IQNA) – Mtafiti wa historia ya Uislamu amesifu kazi za "thamani" i za mwanazuoni wa Kijerumani-Muingereza Wilferd Madelung aliyefariki hivi karibuni.

Akizungumza na IQNA siku ya Alhamisi, Muhammad Kazim Rahmati, mwanazuoni wa utafiti katika "The Encyclopedia of Muslim World Foundation", alisifu mafanikio ya kitaaluma ya Profesa Madelung.

" Wilferd Madelung alikuwa mtaalamu wa historia na teolojia ya Kiislamu  na madhehebu ya Shia. Kazi zake ni vyanzo vya thamani kwa yeyote anayevutiwa na nyanja hizi," Rahmati alisema.

Kisha akarejea kwenye moja ya kazi za marehemu mwanachuoni iliyoitwa "Urithi wa Muhammad SAW" ambayo inaunga mkono maoni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia ya nani aliyestahiki kumrithi Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

“Kitabu hiki ni miongoni mwa kazi zake muhimu sana katika historia ya Kiislamu, kinatokana na uchunguzi wa kina wa simulizi kuu zinazoelezea kipindi cha mwanzo cha Uislamu (tangu kifo cha Mtume  SAW hadi uongozi wa Imam Ali AS) na jinsi mielekeo na masuala mbalimbali yalivyoijenga jamii ya Kiislamu wakati huo. Pia kitabu hicho kinachambua jinsi makundi mbalimbali yalivyoripoti matukio ya kihistoria ili kuficha jukumu lao au kuwalaumu wapinzani wao," mwanazuoni huyo wa Iran aliongeza.

Ripoti nyingi za kihistoria kutoka nusu ya kwanza ya karne ya kwanza Hijria Qamaria zina upendeleo na kuathiriwa na maslahi mbalimbali, alisema, akibainisha kuwa "ili kuelewa kile kilichotokea, tunahitaji kulinganisha maandiko tofauti na kuangalia vyanzo vyake."

"Wasomi wa Ujerumani na wataalamu wa mashariki wamefanya kazi kubwa katika suala hili. Wametumia vyanzo vya asili vya Shia na vyanzo vingine katika masomo yao ya Uislamu na Iran," Rahmati alisema.

Muhammad Kazim Rahmati, a research scholar in The Encyclopedia of Muslim World Foundation, speaks to IQNA on May 11, 2023.

Wilferd Madelung alizaliwa mnamo Desemba 26, 1930, huko Stuttgart, Ujerumani. Alimaliza elimu yake ya msingi na sekondari hapo kisha akahamia Chuo Kikuu cha Cairo, ambako alipata Shahada ya Awali (B.A.) katika Historia na Fasihi ya Kiislamu mnamo 1953.

Aliendelea na elimu yake ya juu nchini Ujerumani na kupata Shahada ya Uzimavi au  PhD ya Masomo ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Hamburg mwaka wa 1957. Tasnifu yake ilisimamiwa na wasomi wa Kiislamu wa Ujerumani R. Strothmann na B. Spuler. Alifanya kazi kama mshiriki wa kitamaduni wa Ujerumani Magharibi huko Baghdad kwa miaka mitatu (1958 - 1960) na kisha akajitolea maisha yake ya kitaaluma kwa Masomo ya Kiislamu. Profesa Madelung amekuwa na nafasi muhimu katika kuarifisha Ushia katika duru za Kiakademia barani Ulaya.

Amechangia pakubwa katika kuendeleza elimu kuhusu fikra na historia ya Kiislamu, hususan madhehebu ya Shia, kwa kuandika na kuhariri takriban vitabu 200 na makala katika majarida ya utafiti na encyclopedia na kuhakiki na kutambulisha vitabu 160. Kazi zake zinashughulikia mada mbalimbali kama vile theolojia, historia, fiqh, madhehebu za Kiislamu, wasifu na bibliografia. Baadhi ya kazi zake zimetafsiriwa kwa Kiajemi.

3483527

captcha