IQNA

Uislamu unaenea

Padri Mkatoliki Hilarion Heagy amesilimu

19:29 - February 28, 2023
Habari ID: 3476641
TEHRAN (IQNA) – Padre Hilarion Heagy, padre mashuhuri wa Kanisa Katoliki la Mashariki lenye makazi yake Marekani amesilimu, akielezea uamuzi wake kama "kurejea katika Uislamu" na kwamba hatua yake ilikuwa "sawa na kurudi nyumbani."

Padri huyo anayeishi California hapo awali alikuwa Mwothodoksi wa Kirusi, akiwa amejiunga na Kanisa Othodoksi la Antiokia mwaka wa 2003, kabla ya kuondoka mwaka wa 2007 na kuhamia Kanisa Katoliki la Mashariki. Alihitimu katika chuo cha mapadri cha Holy Resurrection Monastery  huko St. Nazianz huko Wisconsin na kuwa padre wa Kikatoliki wa Byzantine.

Hata hivyo, katika chapisho lake la blogu, Heagy ambaye kwa sasa anajulikana kama Said Abdul Latif alisema: "Baada ya miongo kadhaa ya kuhisi kuvutiwa na Uislamu kwa viwango tofauti, hatimaye niliamua kuingia."

Abdul Latif alisema kuhusu kusilimu kwake kwamba ilikuwa ni "Kurejea Mashariki" na kurudi kwenye "utambulisho wake wa asili," akitoa maelezo kwa kunukuu Qur'ani Tukufu:

“Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo.." (7:172)

"Ni kwa sababu hii kwamba wanaosilimu mara nyingi hawazungumzii sana 'uongofu' kwani wanazungumzia 'kurejea' kwa Uislamu — imani yetu ya awali. Ni mchakato mrefu wa Kurejea," aliandika.

Kwa kujibu hatu ya padre huyo kuukumbatia Uislamu, makala ya hivi majuzi ya Catholic.com yenye anuani ya, "Safari ya Huzuni ya 'Padri wa Kiislamu'. Habari za kasisi huyo wa zamani kuukubali Uislamu pia zimepokelewa kwa hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii, huku Waislamu wakimkaribisha katika imani na baadhi ya Wakristo wakimsuta kwa "kuritadi."

3482635

captcha