IQNA

Turathi za Kiislamu

Misikiti mitano ya kihistoria ikiwemo ya enzi ya Mtume SAW kukarabatiwa

11:45 - September 01, 2022
Habari ID: 3475715
TEHRAN (IQNA) – Misikiti mitano ya kihistoria inayohusiana na zama za Mtume Muhammad (SAW) katika eneo la Makka itakarabatiwa.

Mradi wa Maendeleo ya Misikiti ya Kihistoria unalenga kuangazia utamaduni tajiri wa Uarabuni, kulinda na kukarabati misikiti, kuiwezesha kudumu zaidi, na kudumisha usanifu wao ambao umeathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa katika karne zilizopita.

Msikiti wa Al-Baiah, uliojengwa na Khalifa wa Abbas Abu Jafar Al-Mansour karibu na Jamarat Al-Aqaba huko Mina, ni msikiti wa kwanza kukarabatiwa Makka kama sehemu ya awamu ya pili ya mradi huo.

Misikiti miwili huko Jeddah - Msikiti wa Abu Inbeh huko Harat Al-Sham na Msikiti wa Al-Khadr kwenye Mtaa wa Al-Dhahab katika kitongoji cha Al-Balad - pia ni sehemu ya mradi wa ukarabati.

Msikiti wa Abu Inbeh ulijengwa zaidi ya miaka 900 iliyopita wakati Msikiti wa Al-Khadr, karibu kilomita 66 kutoka Msikiti Mkuu wa Makka, ulijengwa karibu miaka 700 iliyopita.

Msikiti wa Al-Fath katika eneo la Al-Jamoum pia umepangwa kuendelezwa chini ya mradi huo. Inasemekana kuwa Mtume Muhammad (SAW) alikuwa akiswali katika msikiti huu katika mwaka alioiteka Makka.

Msikiti wa Al-Jubail, ambao ulijengwa zaidi ya miaka 300 iliyopita, pia ni sehemu ya mradi huo na eneo lake la baada ya ukarabati litakuwa mita za mraba 310.

Jumla ya misikiti 30 itajumuishwa katika awamu ya pili ya mradi wa maendeleo unaojumuisha mikoa yote nchini Saudi Arabia.

3480291

captcha