IQNA

Chakula Halali katika Michezo ya Olimpiki Brazil

23:48 - August 06, 2016
Habari ID: 3470499
Michezo ya Olimpiki mwaka 2016 imeanza Jumamosi katika mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil huku wanariadha Waislamu wakihakikishwa kupata chakula halali.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano ya mwaka huu yanashirikisha wanariadha kutoka nchi 208 ambao watashindana katika michezo zaidi ya 40.

Kuwapa wanariadha Waislamu chakula halali kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu ni moja ya suala lililopewa umuhimu mkubwa na waandalizi wa mashindano ya mwaka huu ya Olimpiki nchini Brazil.

Kituo cha Kiislamu cha Brazil, kwa muda wa miezi 8, kimekuwa na mikutano na wawakilishi wa nchi kadhaa kwa lengo la kutayarisha chakula halali kwa wanariadha au wanamichezo Waislamu katika mashindano hayo.

Kituo cha Kiislamu cha Brazil kilitayarisha mapendekezo maalumu kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kuhusu kuhakikisha Waislamu wanaoshiriki katika michezo ya Olimpiki Rio de Janeiro wanapata chakula kilichotayarishwa kwa msingi wa Uislamu.

Kwa mujibu wa taarifa, kutakuwa na milo 65000 kwa siku kwa ajili ya wanariadha 18,000 ambapo milo 8000 itakuwa maalumu kwa ajili ya Waislamu huku ikiwa na nembo ya Halal.

Mbali na wanamichezo, Waislamu wengine wote waliosafiri Rio wanaweza kula chakula halali katika migahawa maalumu ya mji huo.

Chakula Halali katika Olimpiki kitayayarishwa chini ya usimamizi wa Kituo cha Kiislamu cha Brazil. Kituo hicho kinasimamiwa na Hujjatul Islam Sheikh Talib Kharzaji, ambaye amekuwa akihubiri Uislamu Brazil kwa muda wa miaka 27.

Uislamu uliingia Brazil kwa mara ya kwanza kupitia watumwa kutoka Afrika na kisha kutoka wahamiaji wa Lebanon na Syria na inakadiriwa kuwa Waislamu ni asilimia moja hivi ya watu wote milioni 162 katika nchi hiyo.

3460608


Chakula Halali katika Michezo ya Olimpiki Brazil

Chakula Halali katika Michezo ya Olimpiki Brazil

Chakula Halali katika Michezo ya Olimpiki Brazil

Chakula Halali katika Michezo ya Olimpiki Brazil

Chakula Halali katika Michezo ya Olimpiki Brazil


Chakula Halali katika Michezo ya Olimpiki Brazil





captcha