Mkurugenzi wa IQNA, Hamid Saber Farzam alipokoa cheti cha heshima kwa mnasaba wa ushindi huo katika hafla iliyofanyika Ijumaa jioni mjini Tehran.
Maonyesho ya 21 ya Habari na Mashirika ya Habari yalifunguliwa rasmi Jumapili iliyopita mjini Tehran katika sherehe iliyohudhuriwa na Rais Hassan Rouhani.
Maonyesho hayo yalishiriksha vyombo 700 vya habari vya kitaifa. Aidha kuna washiriki kutoka Ujerumani, Italia, Marekani, China , Ufaransa, Uturuki, Kuwait, Lebanon, Japan, Iraq na Russia. Maonyesho hayo yanaendelea hadi Novemba 13 chini ya kauli mbiu ya 'Ukosoaji wa kiadilifu na uwajibikaji."