IQNA

Utawala wa Israel

Qatar yapinga pendekezo la kufunguliwa ofisi ya ubalozi wa Israel mjini Doha

22:49 - September 13, 2022
Habari ID: 3475777
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Qatar imepinga ombi la utawala haramu wa Israel la kuanzishwa ubalozi mdogo wa muda wa Israel mjini Doha katika kipindi cha kufanyika fainali za soka za Kombe la Dunia la FIFA 2022.

Vyombo vya habari vya utawala ghasibu wa Israel hivi karibuni viliripoti kuwa, kumekuweko mazungumzo baina ya viongozi wa utawala huo na wenzao wa Qatar kwa ajili ya kufunguliwa ubalozi mdogo wa muda wa Israel ambao utakuwa maalumu tu katika kipindi cha kufanyika mashindano ya soka ya kombe la Dunia.

Hata hivyo duru za Israel zinasema kuwa, viongozi wa Qatar wamepinga na kukataa ombi hilo ambalo kwa mujibu wa viongozi wa Tel Aviv lililenga kufungua ubalozi wake mdogo wa muda mjini Doha kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali ya mashabiki wa Israel ambao wataelekea nchini humo kwa ajili ya kushuhudia mashindano hayo.

Baadhi ya duru za utawala ghasibu wa Israel zimetangaza kuwa, mazungumzo baina ya pande mbili kuhusiana na kadhia hiyo yangali yanaendelea ingawa viongozi wa Qatar hawaonyeshi kulipokea vizuri ombi hilo la Israel.

Makumi ya maelfu ya mashabiki wa soka Wazayuni wanatarajiwa kuwa miongoni mwa mashabiki mbalimbali wa soka ulimwenguni watakaoelekea Qatar kwa ajili ya kushuhuhudia mashindano ya soka ya Kombe la Dunia.

Mechi za hatua ya makundi za Kombe la soka la Dunia la Qatar 2022 zitafanyika kuanzia Novemba 20 hadi Desemba 2, hatua ya timu16 itaanza Desemba 3 hadi 6, robo fainali itafanyika Desemba 9 na 10, nusu fainali tarehe 13 na 14 za mwezi huo, na fainali ya mashindano hayo itafanyika tarehe 18 Desemba.

alalam.ir

captcha