IQNA

Fikra za Kiislamu

Tawba: Njia ya Mwanadamu kubaki na Matumaini

22:42 - September 13, 2022
Habari ID: 3475776
TEHRAN (IQNA) – Kila mtu anaweza kukosea na kufanya madhambi lakini ipo njia ya kurejea kwa Mwenyezi Mungu na kuomba msahamah kwani Yeye hawaachi waja wake hata iweje.

Tawba (toba) maana yake ni kurudi kutoka katika dhambi. Katika Quran na maandiko mengin ya kidini, mara nyingi imekuwa ikihusishwa na Mwenyezi Mungu.

“…Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu.”( Surah At-Tawbah, sehemu  ya Aya ya 118)

Tawwab  ni  moja ya majina la Mwenyezi Mungu ambalo maana yake ni yule anayerejesha (kitu) mara kwa mara.

Tawba ni njia ya mtu kurejea kwa Mwenyezi Mungu, na njia hii daima iko wazi, hata kama atafanya makosa mara kwa mara. Bila shaka ni lazima kwamba Tawba lazima iwe halisi.

Tawba halisi ina masharti na hatua fulani ambazo ni pamoja na: majuto, nia thabiti ya kuacha madhambi, na kufidia dhambi iliyotendwa. Hapo ndipo mtu anaweza kuwa na Tawba halisi.

Mwenyezi Mungu anawaita waumini wawe na Tawba kama hii: “ Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.’” (Sura At-Tahrim, Aya ya 8).

Moja ya mambo ya kwanza waliyoyafanya wajumbe wote wa Mungu ni kuwaalika watu watubu, kwa sababu bila hivyo na bila ya kukaa mbali na dhambi, kusingekuwa na mahali pa kumwalika mtu kwenye tauhidi na wema.

Nabii Hud (as) alipoteuliwa kuwa utume aliwaambia watu wake: “Na enyi watu wangu! Muombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika, na atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu. Wala msigeuke mkawa wakosefu. (Surah Hud, Aya ya 52)

Hivyo ndivyo alivyofanya Nabii Shuaib (AS) pia: “Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kurehemu na Mwenye upendo.” (Surah Hud, Aya ya 90)

Tawba si kwa ajili ya baadhi ya watu au kwa ajili ya makundi fulani ya watu. Ni kwa ajili ya kurudi kutoka katika dhambi zote. Ni njia ya kuonyesha majuto na kumwomba Mungu msamaha. Tawba ni fursa iliyotolewa na Mungu kwa kuweka matumaini katika mioyo ya watu.

captcha