IQNA

Wahusika wa Karbala /2

Wale walioshindwa kufuatana na Imam Hussein AS katika siku ya Ashura

13:47 - September 12, 2022
Habari ID: 3475769
TEHRAN (IQNA) -Vita vya Karbala vinaleta mafunzo mengi. Miaka 1383 iliyopita tarehe 10 Muharram katika siku ya Ashura, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala katika Iraq ya leo.

Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili ili kuilinda dini ya Allah. Hamasa ya Karbala ilikuwa dhihirisho la mambo mawili makuu. Kwanza ni ujasiri, ushujaa, moyo wa kujitolea, uaminifu pamoja na kuyapokea kwa moyo mkunjufu mauti ya kuuawa shahidi, sifa walizojipamba nazo wapiganaji wachache wa jeshi la haki wakiongozwa na Imam Hussein AS dhidi ya Yazid bin Muawiya.

Katika mapambano hayo ya Karbala, misimamo ya watu binafsi ilidhihirika wazi kulingana na matendo na machaguo yao.

Kundi moja la watu nusura likose nafasi ya kuandamana na Imam Hussein (AS) siku hiyo.

Watu hawa hawakumpinga Imam Hussein (AS). Dahhak ibn Abd Allah al-Mashriqi alikuwa mmoja wa watu hawa waliokuja Karbala kama sahaba wa Imam Husein (AS) na hata kubakia hapo hadi alasiri ya Ashura lakini walitoroka katika dakika za mwisho za mapambano.

Alikuwa amemuahidi Imam Hussein (AS) kwamba angekaa kwenye kambi hiyo mradi tu angeweza kufanya jambo fulani. Wakati masahaba wengi wa Imam Hussein (AS) walipouawa shahidi Siku ya Ashura na ikadhihirika wazi kwamba Imam Hussein (AS) pia alikuwa anaelekea kuuawa shahidi, Dahhak alitoroka eneo hilo. Yamkaini kitendo chake kilikuwa cha busara kwani alikua mmoja wa wasimuliaji wa kile kilichotokea huko Karbala. Nia yake ya kweli ya kutoroka na nafasi yake huko Akhera haiko wazi lakini kwa hakika alikuwa n msimamo tofauti kulinganisha na wale masahaba ambao waliuawa kishahidi huko Karbala.

Mtu mwingine katika kundi hili ni Al-Tirimmah ibn Adi. Alikuwa Shia na sahaba wa Imam Ali (AS). Ameelezewa kama mshairi shujaa na mzungumzaji ambaye alikuwa mjini Kufa wakati wa matukio ya Karbala. Wakati Imam Hussein (AS) alipokabiliana na askari wa Al-Hurr b. Yazid al-Riyahi, Al-Tirimmah alijiunga na jeshi la Imam na kutoa habari mpya kutoka Kufa.

Alimwambia Imam Hussein (AS) kwamba haoni uwezekano wa kufaulu huko Kufa, akimshauri Imam kwenda Yemen lakini Imam Hussein (AS) alikataa pendekezo lake. Kisha Al-Tirimmah akamwomba Imam amruhusu aende kwa familia yake huko Kufa na awape baadhi ya vifaa na pesa na Imam akakubali, akamwambia afanye hivyo na arudi mara moja. Alikwenda Kufa na alipokuwa anarudi, akapokea habari za kifo cha kishahidi cha Imam. Alijutia uamuzi wake.

Yeye ni mmoja wa walionusurika lakini kama angekuwa na ujuzi wa kina, angechagua kitendo cha ‘wajib zaidi’ badala ya cha wajib. Aliweza kumwambia Imam kwamba alikuwa tayari kufanya kila kitu kwa ajili ya harakati zake.

Makala haya yalikuwa ni muhtasari wa matamshi yaliyotolewa na Hujjatul Islam Mohammadreza Jabbari, profesa wa historia ya Kiislamu.

captcha