IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu Ujerumani

22:35 - August 18, 2022
Habari ID: 3475642
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Kupambana na Itikadi Kali ya Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar imesema imeashiria ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani, na kusema hilo limeenda sambamba na kushadidi mashambulizi ya vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia dhidi ya Waislamu.

Idara hiyo ya Kituo cha Kiislamu Al Azhar nchini Misri, imechapisha ripoti huku likiashiria ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani na kutangaza kuwa, kueneza chuki dhidi ya watu wa dini za waliowachache na wahajiri ni suala lililokita mizizi barani Ulaya na limeongezeka katika miaka ya hivi karibuni katika nchi nyingi za Ulaya. Kwa mujibu wa ripoti hii, Kamati ya Ulaya ya kupambana na ubaguzi wa rangi na chuki katika Bunge la Ulaya pia imekiri kuwepo tatizo hilo.

Idara ya Kupambana na Itikadi Kali ya Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar iliongeza kuwa: katika nchi zinazozungumza Kijerumani, zikiwemo Ujerumani, Austria na Uswizi; Kurasa za mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram na Twitter ndio jukwaa muhimu zaidi la kueneza kauli za chuki dhidi ya wahajiri na hasa Waislamu.

Kauli hizi mara nyingi hutoka kwa vyama vya mrengo wa kulia. Kwa kuwa Waislamu kwa ujumla ni wahamiaji na wana mila na desturi tofauti na jamii ya Wajerumani, maneno ya chuki dhidi ya wageni na wakimbizi mara nyingi yanaelekezwa kwa Waislamu. Vyama vya mrengo mkali wa kulia nchini Ujerumani, huku vikidai uzalendo, vinataka kuzuia kuenea Uislamu katika nchi za Magharibi.

Kulingana na ripoti hii, mnamo 2020, kesi 1,026 utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu ziliripotiwa nchini Ujerumani, ambapo wenye misimamom mikali ya mrengi wa kulia walihusika na  kesi 945. Katika mwaka 2021, ingawa takwimu rasmi za mashambulio dhidi ya Waislamu zilipungua hadi kesi 732, wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia  ilihusika na kesi 588.

Wataalamu wanaamini kwamba idadi halisi ya mashambulizi ni kubwa zaidi na imeongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita, hata hivyo, mashambulizi haya hayajasajiliwa rasmi.

 Baadhi ya Waislamu wamezungumza kuhusu chuki dhidi ya Uislamu iliyoanzishwa katika taasisi za mahakama za Ujerumani pamoja na polisi nchini humo.

4078980

captcha