IQNA

Waislamu na Wakristo Misri

Al-Azhar yatoa risala za rambirambi kufuatia ajali mbaya ya moto kanisani Misri

16:45 - August 15, 2022
Habari ID: 3475626
TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar Misri kimetoa salamu za rambirambi kwa Wakristo nchini humo kutokana na moto kanisani uliosababisha vifo vya takriban watu 41 wakiwemo watoto.

Al-Azhar na Imamu wake Mkuu Ahmed El-Tayeb walitoa rambirambi zao za dhati na pole kwa Kiongozi wa Kanisa la Kopti n Papa Tawadros II na Wakristo wote nchini Misri kutokana na mkasa huo wa moto.

Sheikh El Tayeb amesema Al-Azhar na wanachuoni wake na mashekhe wote wanasimama pamoja na ndugu zao Wakristo katika ajali hii mbaya na kutoa pole kwa familia za waliopoteza maisha. Sheikh El-Tayyeb alielezea utayari wa Al-Azhar kutoa msaada wa pande zote kwa majeruhi na utayari wa hospitali za Al-Azhar kuwapokea majeruhi wakati wa kutoa msaada wa kisaikolojia kwao.

Moto uliosababishwa na tatizo la umeme ulikumba kanisa la Kikristo la Coptic la Misri wakati wa Misa siku ya Jumapili, na kusababisha mkanyagano na kuua takriban watu 41, wengi wao wakiwa watoto na wengi wakiugua kwa kuvuta moshi.

Moto huo ulianza kabla ya saa tatu asubuhi katika Kanisa la Abu Sifin katika mji wa Giza ambapo takriban watu 1,000 walikuwa wamekusanyika.

Moto huo uliziba lango la kuingilia kanisani, na kusababisha mkanyagano, vyanzo hivyo viwili vilisema, na kuongeza kuwa wengi wa waliouawa walikuwa watoto.

Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri naye ametuma salamu zake za rambi rambi kufyuatia tukio hilo na ameamuru mashirika yote ya kiserikali kuchukua hatua za kutoa huduma zinazohitajika baada ya maafa hayo.

Kanisa la Koptik nchini Misri limethibitisha kuwa watu 41 wamepoteza maisha na wengine 14 wamejeruhiwa katika tukio hilo. Idara ya Mwendesha Mashtaka Misri imetangaza kuanza uchunguzi.

Wakopti ni idadi kubwa zaidi ya jamii ya Wakristo katika nchi ya Kiarabu ambapo idadi yao ni milioni 10 kati ya watu milioni 103 nchini humo. 

3480099

captcha