IQNA

Imam Ridha AS

Mwanafunzi wa Kiafrika wahudhuria warsha katika Haram ya Imam Ridha AS

22:18 - August 11, 2022
Habari ID: 3475607
TEHRAN (IQNA) – Idaraya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha AS katika mji wa Mashhad nchini Iran imeandaa duru ya tisa ya warsha kwa mabalozi wake ambapo duru hii imewajumuisha wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Madagascar.

"Wahadhiri wanaozungumza Kifaransa wameendesha duru ya sasa ya warsha iliyofanyika kuanzia Agosti 7-11 na washiriki wametunukiwa vyeti baada ya kukamilisha warsha", alisema Naibu wa Masuala ya Kimataifa katika kitengo  Elimu na Utamaduni chaidara hiyo , akibainisha kuwa wanafunzi 35 wa Madagascar na wanaharakati walishiriki.

Kwa mujibu wa Seyyed Mohammad Zolfaghari, aina mbalimbali za programu ziliangaziwaa katika duru hii ya warsha kama vile kozi za mafunzo, kutembelea maeneo mbali mbali ya Haram, kushiriki katika maombolezo ya Muharram, mafunzo kuhus maisha na mwenendo wa Imam Hussein  AS.

Alitaja lengo la duru ya hivi karibuni ya warsha kuwa ni kujua maisha na mwenendo wa Imam Ridha AS, shughuli za kielimu na kitamaduni na uwezo wa Haram, kuanzisha uhusiano mzuri na vituo vya kitamaduni na wanaharakati, na kuwawezesha wapanue mtandao wao wa kimataifa.

Ameongeza kuwa warsha hizo za hivi karibuni pia zililenga kuwafahamisha washiriki mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. "Tunatumai kwamba wanafunzi hawa wachanga na wanaharakati wa kitamaduni wanaweza kuleta madiliko chanya barani Afrika katika siku zijazo".

3480049

captcha