IQNA

Zaidi ya watu milioni 6 walizuru Karbala siku ya Ashura

21:41 - August 11, 2022
Habari ID: 3475606
TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa mamlaka za Iraq, zaidi ya wafanyaziarai milioni sita walitembelea maeneo matakatifu ya Karbala siku ya Jumanne, Siku ya Ashura.

Ali al-Mayalee, naibu gavana wa Karbala, alisema kuwa idadi ya wafanyaziara waliofika mjini humo Jumanne ilikuwa takribani milioni sita.

Alisema kutokana na hatua za usalama zilizochukuliwa, hakuna tukio la uvurugaji usalama lililoripotiwa wakati wa mjumuiko wa maombolezo ya Siku ya Ashura ya kukumbuka kuuawa  shahidi Imam Hussein AS.

Zaidi ya maafisa 30,000 walipewa jukumu la kulinda usalama wa mjumuiko huo wa aina yake.

Pia, idadi ya wafanyaziara katika mji wa Kadhimiya siku hiyo hiyo inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni mbili.

Haya ni kwa mujibu wa Sa’d al-Hajieh, naibu katibu wa Mfawidhi wa wa maeneo matakatifu ya Al-Kadhimiya. Naye pia alibainisha kuwa maandamano ya maombolezo yalifanyika katika mazingira salama kabisa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iraq, zaidi ya wafanyaziara 17,000 wa kigeni walikuwa wamewasili katika nchi hiyo ya Kiarabu kabla ya kuanza kwa mjumuiko huo mkubwa.

Ashura ni siku ya kumi ya Muharram, mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwandamo ya Hijri.

Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengine katika sehemu mbalimbali za dunia, kila mwezi wa Muharram hushirki katikamijumuko ya kuomboleza katika kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba zake.

Imam huyu  wa tatu wa  Waislamu wa madhehebu ya Shia  akiwa na  kikundi kidogo cha wafuasi wake na wanafamilia waliuawa shahidi na kidhalimu mtawala wa kiimla na katili wa zama hizo - Yazid Bin Muawiya, katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria.

3480051

captcha