IQNA

Waislamu Russia

Rais wa Chechenya: Rais Putin anaiheshimu Qur’ani Tukufu

20:31 - July 29, 2022
Habari ID: 3475553
TEHRAN (IQNA)- Ramzan Akhmadovich Kadyrov, Rais wa Jamhuri ya Chechenya ndani ya Shirikisho la Urusi amesema Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo anaiehsmu sana Qur’ani Tukufu.

Katika klipu aliyosambza katika mitandao ya kijamii ameandika kuwa: “Putin husoma Qur’ani Tukufu na katika maktaba yake binafsi ana nakala ya Kitabu Hicho Kitakatifu.”

Kadirov ametoa tamko hilo hivi karibuni na kuongeza kuwa Rais Putin hunukulu aya za Qur’ani anapokutana na viongozi wa kimataifa. Kadirov ameendelea kusema kuwa: “Kwetu sisi Waislamu wa Russia,  kuwa na rais ambaye hunukulu aya za Qur’ani ni jambo lenye kutuletea fakhari ya kweli.”

Aidha Rais wa Jamhuri ya Chechenya ameendelea kubaini kuwa: “Sisi tunafuraha kuwa na kiongozi kama huyo mwenye kupenda taifa, mcha Mungu, muadilifu na mwenye busara.”

Ikumbukwe kuwa, mwaka 2015,Rais Vladimir Putin wa Russia alimtunuku Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali hamenei, nakala ya zamani yenye thamani kubwa ya Qur'ani Tukufu.

Kadyrov aliteuliwa na Rais Putin mwaka 2007 kuongoza eneo la Jamhuri ya Chechnya ambalo aghalabu ya wakaazi wake ni Waislamu na amekuwa mstari wa mbele kuhuisha Uislamu eneo hilo kwa kujenga misikiti na harakati nyinginezo.

Idadi ya Waislamu nchini Urusi inakadiriwa kuwa watu milioni 25 kati ya watu milioni 145 nchini humo.

Ahalabu ya Waislamu nchini Russia wanaishi katika mji mkuu Moscow na miji mingine mikubwa kama vile St. Petersburg and Yekaterinburg. Halikadhalika kuna idadi kubwa ya Waislamu maeneo kama vile Jamhuri ya Tatarstan, Jamhuri ya Bashkortostan, Jamhuri za Caucasus Kaskazini, Jamhuri za Caucasus au Kavkazia Kaskazini , Jamhuri ya Adygea, Jamhuri ya Chechnya, Jamhuri ya Dagestan, Jamhuri ya Ingushetia, Jamhuri ya Kabardino-Balkaria, Jamhuri ya Karachay-Cherkessia, Jamhuri ya Krasnodar Krai na Jamhuri ya Ossetia Kaskazini

 Jamhuri zote hizo ziko katika Shirikisho la Urusi lakini zina mamlaka ya ndani ya kujitawala.

4074025

captcha