IQNA

Uchambuzi wa kisiasa

Malengo ya safari ya Biden Asia Magharibi, kuanzia uhusiano wa Israel-Saudia hadi soko la nishati

12:43 - July 06, 2022
Habari ID: 3475468
TEHRAN (IQNA) - Kwa mujibu wa mtaalamu kutoka Ujerumani, mazungumzo kuhusu bei ya nishati na vile vile kutetea uhusiano wa kawaida kati ya Saudi Arabia na utawala wa Israel ni kati ya ajenda ya ziara ya kwanza ya Rais wa Marekani Joe Biden katika eneo la (Asia Magharibi) Mashariki ya Kati.

Biden atafanya ziara yake ya kwanza katika eneo la Asia Magharibi Julai 13 kama rais wa Marekani. Anatazamiwa kuzuru Saudi Arabia na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa zilizopachikwa jina bandia la Israel wakati wa safari hiyo. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, mbali na masuala la soko la nishati yaani sekta za mafuta ya petrol na gesi, masuala mengine kama vile mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama JCPOA na mgogoro wa Yemen yako kwenye ajenda za safari hiyo.

Ili kujadili safari hiyo, Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani ( IQNA) limewasiliana na Daktari. Mark Furness, mtafiti mkuu katika mpango wa utafiti wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Taasisi ya Maendeleo na Uendelevu ya Ujerumani (IDOS).

Katika mahojiano na IQNA, alizungumza juu ya malengo na athari za safari ijayo ya Joe Biden Mashariki ya Kati.

IQNA: Katika siku za hivi karibuni, tumeona maoni mengi kuhusu sababu za safari ijayo ya Joe Biden nchini Saudi Arabia. Kwa maoni yako, Biden anafuatilia nini katika safari hii.

Furness: Inaonekana sababu kuu zinahusiana na masuala ya mikakati ya kijiografia  (jiostratijia) – Russia innatekeleza oparesheni ya kijeshi Ukraine na uhusiano wa China na Marekani uko katika hali ya taharuki. Safari hiyo inathibitisha tena kwamba Saudi Arabia ni mshirika wa muda mrefu na mshirika wa kimkakati wa Marekani, na katika hali ya sasa ya kijiostratijia duniani Marekani imeamua  kupuuza ukiukaji wa haki za binadamu ya Saudia.

Zaidi ya hayo ni ukweli kwamba bei ya nishati yaani mafuta ya petrol na gesi imesukumwa juu sana na oparesheni za kijeshi za Russia nchini Ukraine. Kwa upande mmoja Marekani inatazamiwa kuchukua nafasi kama muuzaji mkuu wa nishati kwa bara Ulaya katika miaka michache ijayo na kwa upande mwingine bei ya juu ya nishati inasababisha mfumuko wa bei, ambayo itaathiri vibaya nafasi ya Biden kuchaguliwa tena.

Bei ya juu ya mafuta na gesi imebatilisha athari za vikwazo vya kifedha dhidi ya Russia pia. Kwa hivyo, ingawa Biden amesema hatashinikiza ongezeko la uzalishaji wa mafuta ghafi ya petroli kuna uwezekano wa kuwa na mjadala mkubwa kuhusu jinsi ya kurejesha bei ya nishati chini, sio tu baina ya pande mbili na Saudis lakini pia na wanachama wengine wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.

IQNA: Baadhi wanaamini kuwa serikali ya Joe Biden inalengo kuishinikiza au kuihimiza Saudi Arabia kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Israel. Je, unadhani kuna ukweli katika hilo.?

Furness: Hilo ni swali zuri. CNN ilibaini kuwa kuna ishara kwamba ndege rasmi ya Rais wa Marekani inayojulikana kama Air Force One itaruka moja kwa moja kutoka Tel Aviv hadi Jeddah. Umoja wa Falme za Kiarabu na Morocco zimeanzisha na uhusiano wa kawaida na Israel, na inaonekana Iran inafuatilia kwa karibu jinsi uhusiano wa Saudi na Israel unavyoendelea. Nimesoma kwamba Wamarekani wamekuwa wakifuatilia kadhia ya kuwepo uhusiano wa karibu wa Israel na Saudi lakini sioni tangazo kuu kama matokeo ya safari.

Saudi Arabia na Israel zina mtandao mzuri wa mawasiliano ya nyuma ya pazia kuhusiana na masilahi yao ya kawaida.

IQNA: Je, Ulaya ina maoni gani kuhusu safari ya Biden nchini Saudi Arabia, na je, safari hiyo na makubaliano yatakayofikiwa yatakuwa kwa manufaa ya Ulaya, kutokana na vita vinavyoendelea nchini Ukraine?

Furness: Sijaona maoni yoyote maalum kutoka kwa viongozi wa Ulaya kuhusu safari ya Biden, hasa ikizingatiwa kuwa aliiita Saudi Arabia 'dola la kihuni' sio muda mrefu uliopita. Nadhani watawala wa Ulaya wanaona mantiki jiostratijia nyuma ya safari.

Mambo mengine mawili ambayo serikali za Ulaya zinaweza kuthamini ni uwezekano wowote wa kurejesha makubaliano ya nyuklia ya Iran (JCPOA), ingawa uwezekano bado ni mdogosana, na kuendelea kwa usitishaji mapigano nchini Yemen, ambayo baadhi ya vyombo vya habari vimedai kuwa nia Mrithi wa Ufalme wa Saudia, Mohammad bin Salman (MBS) ni kuonyesha Biden kuwa anataka kutatua kadhia hiyo.

Bila shaka, matokeo yoyote ambayo yanapunguza bei ya nishati yatakuwa kwa manufaa ya Ulaya.

IQNA: Je, unafikiri kwamba safari ya Biden nchini Saudi Arabia inaweza kuwa na nafasi katika masuala kama vile kumalizika kwa vita vya Yemen na kurejeshwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tehran na Riyadh?

Furness: Sioni mahusiano kati ya Tehran na Riyadh yakibadilika hivi karibuni, ingawa nimesikia kwamba kumekuwa na mawasiliano ya muda hivi karibuni.

Marekani itafurahi kwamba Wasaudi na Wairani wanazungumza, lakini inaonekana kwamba kila mtu anajiandaa kwa usawa mpya wa kikanda ambapo JCPOA haipo mezani tena na kila mtu anajaribu kudhibiti ushawishi wa Iran.

Kuhusiana na Yemen, hakuna uwezekano kwamba vita ‘vitakwisha’ hivi karibuni. Mgogoro huo uko kwenye ajenda ya mazungumzo huko Jeddah, na baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kwamba MBS alihusika  katika kuongeza muda wa usitishaji mapigano, ambao nadhani lazima ulihusisha baadhi ya mawasiliano na Tehran. Kwa hivyo Biden atajaribu kufanya maendeleo kwenye maswala yote mawili lakini hatupaswi kutarajia miujiza.

IQNA: Unadhani hatima ya mazungumzo ya JCPOA itakuwa ipi, na ni nini nafasi ya Ulaya katika kurejea Marekani kwenye JCPOA?

Furness: Umoja wa Ulaya na serikali za Ulaya zimekuwa zikijaribu kuirejesha Marekani kwenye meza na wataendelea kufanya hivi, kwa sababu hakutakuwa na mapatano yoyote bila Marekani.

Tatizo kama ninavyoona ni kwamba madola mengine wote, kama vile Saudi Arabia, Marekani na utawala wa Israel, hawaiamini Iran na wanataka kuifanya Iran kutengwa na kuwa dhaifu. Katika kujibu Irna imesitisha utekelezaji wa baadhi ya vipengee vya JCPOA kuhusu kurutubisha uranium, na utawala wa Israel unajibu  kwa kuwaua wanasayansi Wairani  na mashambulizi ya mtandaoni.

 

Tuna tatizo la usalama. Mimi si shabiki wa serikali ya Iran na siasa zake za kieneo, lakini ukweli unabakia kuwa maadamu Iran inahisi kuna tishio kutoka kwa Majirani zake na Wamarekani, basi itaendeleza mpango wake wa nyuklia. Sidhani kama Iran inaweza kulazimishwa kkaucha mpango huo wa nyuiklia, na sidhani kama mbinu ya uahsama inayotumiwa na majirani Iran itakuwa na ufanisi kwa muda mrefu.

Mahojiano na Mohammad Hassan Goodarzi

Maoni katika mahojiano haya ni yale ya mwenye kuhojiwa pekee na si lazima yawe yanaakisi maoni ya Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani (IQNA)

3479544

captcha