IQNA

Sura za Qur'ani / 10

Sura Yunus: Changamoto kubwa kwa wakanushaji

11:09 - June 27, 2022
Habari ID: 3475431
TEHRAN (IQNA) – Sehemu za aya za Qur’ani zina visa vya Mitume wa Mwenyezi Mungu na makabiliano yao na wale wanaoikadhibisha dini na maamrisho ya Mwenyezi Mungu.

Baadhi ya aya za Surah Yunus zinawaweka kwenye changamaoto watu kama kama hao, hususan wale wanaokanusha  kuwa Qur'ani Tukufu ni Kitabu cha kheri.

Sura nyingi za Qur'ani zimepewa majina ya mitume. Surah Yunus, ni sura ya 10 ya Quran yenye aya 109. Yunus amepewa jina la Nabii Yunus.

Hii ni Sura ya Makki (iliyoteremshwa Makka) na iko katika Juzuu ya 11 ya Qur'ani.

Sura inasimulia kisa cha Nabii Yunus (AS) na watu wake waliookolewa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Inasema kwamba Nabii Yunus (AS) alikwenda kwa watu ili kuwaongoza. Aliwaambia wamwabudu Mungu na kuacha njia zao mbaya, lakini walikataa kusikiliza na hivyo ikabidi aondoke kwa meli. Akiwa baharini alimezwa na nyagumi mkubwa na alikaa ndani ya tumbo la samaki huyo kwa siku kadhaa. Kisha akaokolewa na Mwenyezi Mungu na kutumwa kwa watu hao tena. Wakati huu walikubali utume wake.

Mbali kisa cha Nabii Yunus (AS), Sura hii ina aya zinazosimulia kisa cha baadhi ya Mitume wengine, akiwemo Nabii Nuhu (AS), ujenzi wa meli, na watu walioukadhibisha utume wake kisha Mwenyezi Mungu akawataremeshia dhoruba kuwaadhibu. Vile vile kuna kisa cha Nabii Musa (AS), kulingania Firauni kwa Mwenyezi Mungu, kugombana kwake na wachawi, na kuipasua kwake bahari ili yeye na watu wake wavuke bahari huku Firauni na watu wake wakiwa wamezama.

Sura pia inahusu matatizo ambayo Mtume Muhammad (SAW) alipitia katika kukabiliana na Mushrikeen (washirikina). Mushrikeen walihoji utukufu wa Qur'ani. Hivyo Qur'ani inawapa changamoto ya kuonyesha muujiza kama alivyofanya Mtukufu Mtume Muhammad SAW.

Makusudio ya Sura Yunus  ni kutilia mkazo juu ya Tauhidi. Baadhi ya tafsiri za Qur'ani zinasema kuwa Sura hii iliteremka baada ya baadhi ya Mushrikeen kukanusha suala Wahy na kudai kuwa eti Qur'ani Tukufu ni uchawi.

Mada nyinginezo katika Sura Yunus kama vile dalili za Mwenyezi Mungu, sababu zinazothibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, Wahy, na malengo ya Manabii wa Mwenyezi Mungu..

Baadhi ya aya za Sura Yunus zinaangazia ukaidi wa waabudu masanamu na wapagani na kuwaalika warejee katika njia ya haki. Halikadhalika sura hii inawarejelea kuwa wale wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu wanapokabili matatizo tu na kumsahau wakiwa katika hali ya kawaida.

Habari zinazohusiana
captcha