IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

CAIR yataka FBI ichunguze uteketezaji Moto wa Msikiti wa Minnesota, Marekani

14:18 - June 18, 2022
Habari ID: 3475391
TEHRAN (IQNA)- Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) linataka Idara ya Upelelezi Marekani (FBI) ichunguze tukio la jinai la uteketezaji moto wa msikiti wa East Grand Forks huko Minnesota mapema mwezi huu.

Video ya kamera ya usalama inamuonyesha mshukiwa wa kike, aliyetambuliwa kama Suzette Thompson mwenye umri wa miaka 57 wa Thief River Falls, akitumia kopo la kupulizia na kiberiti cha gesi kuteketeza pazia ndani ya jengo hilo kabla ya kuondoka haraka kwenye eneo la tukio.

CAIR tawi la Minnesota imesema inaunga mkono kuainisha tukio hilo kama uhalifu wa chuki, kufuatia kukamatwa kwa Thompson, ambaye alishtakiwa kwa makosa mawili ya uchomaji moto wa digrii ya kwanza.

"Sisi kama jumuiya tumepatwa na kiwewe," alisema mjumbe wa CAIR-MN Imam Mohammed, "Wanajamii wetu wana hofu."

Ripoti iliyotolewa na CAIR mwezi Aprili  mwaka 2021 ilibaini kuwa Marekani kumeshuhudiwa ongezeko la asilimia 9 ya idadi ya malalamiko ya unyanyasaji dhidi ya Waislamu ambayo yalipokewa mwaka wa 2020 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.

Kwa upande wake Baraza la Jumuiya za Kiislamu nchini Marekani limemwandikia barua Rais wa nchi hiyo, Joe Biden likisisitiza kuwa, kuwepo mwakilishi maalumu wa kusimamia na kupambana na chuki na propaganda chafu dhidi ya Uislamu kunaweza kusaidia juhudi za kupata suluhisho la tatizo hilo ambalo linaizonga jamii ya Waislamu nchini Marekani. 

3479342

Habari zinazohusiana
captcha