IQNA

Nyota wa Man U Paul Pogba asema Uislamu umemfanya awe mtu bora

11:50 - June 12, 2019
Habari ID: 3471997
TEHRAN (IQNA) – Paul Pogba, nyota wa timu ya Manchester United Ligu Kuu ya England nchini Uingereza anasema imani imani yake ya Kiislamu imemfanya awe mwanadamu bora.

Pogba ambaye ni mchezaji wa kiungo cha kati ni miongoni mwa wachezaji ghali zaidi wa soka duniani alijiunga na Machester United mwaka 2016 kutoka Juventus ya Italia ambapo alinunuliwa kwa Euro 105.

Anasema mama yake ni Mwislamu lakini katika familia yake hawakufuata mafundisho ya Kiislamu utotoni. Hatahivyo Pogba anasema baadaye akiwa kijana aliamua kuufuata Uislamu kikamilifu baada ya kuwa na marafiki wenye imani thabiti.

Anaongeza kuwa, kwa ujumla kuna taswira potofu katika vyombo vya habari kuhusu Uislamu. Anaongeza kuwa Uislamu haufungamani na ugaidi kama wengi wanavyodhani katika nchi za Magharibi na kuongeza kuwa: "Kile ambacho tunasikia katika vyombo vya habari ni kinyume cha uhalisia wa mambo kwani Uislamu ni dini maridadi."

Baada ya kupitia kipindi kigumu katika maisha ya binafsi, Pogba alienda kutekeleza ibada ya Umrah katika mji Mtakatifu wa Makka mwaka huu. Anasema: " Sikuzaliwa Mwislamu ingawa mama yangu alikuwa Mwislamu. Nililelewa kwa msingi wa kuwaheshimu wote." Anaongeza kuwa, alikuwa na marafiki wengi na katika mazungumzo nao alianza kujiuliza maswali mengi sammba na na kufanya utaifiti. "Wakati moja niliswali pamoja na marafiki zangu na nilipata hisia nzuri na iliyo tafauti." Anasema baada ya hapo aliamua kusilimu na akawa anaswali sala tano kwa siku. Anabaini kuwa moja ya sababu za kuswali ni kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha na kumshukuru kwa ajili ya afya n.k.

"Uislamu umefungua akili yangu na kunifanya niwe mtu bora. Kila wakati natafakari kuhusu maisha ya akhera," anaongeza.Nyota wa Man U Paul Pogba asema Uislamu umemfanya awe mtu bora

Anasema anawaheshimu watu wote hata kama si Waislamu kwani sote ni wanadamu bila kujali dini au rangi. Mchezaji huo maarufu wa Manchester United, ambaye alizaliwa Ufaransa na anachezea timu ya taifa ya nchi hiyo, anamaliza kwa kusema: "Uislamu unatufunza kuheshimu ubinadamu."

3468726

captcha