IQNA

Nyumba ya mwalimu yatumika kama shule ya wanafunzi 700

Karibu watoto 700 hufika kila siku katika nyumba ya mwalimu Adel al-Shorbagy baada ya kuwa ameibadilisha nyumba kati katika mji wa Taiz nchini Yemen kuwa shule. Mji huo umekuwa ukishambuliwa kwa mabomu ya ndege za kivita za Saudia.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuipundua serikali ya nchi hiyo. Vita hivyo vimesababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasiopungua 15,000 wasio na hatia. Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa walipoteza maisha huku miundo msingi ya nchi hiyo kama vile shule, mahospitali, madaraja n.k ikiharibiwa kabisa.