Mohammad Talal al-Farsi, mkuu wa kituo taasisi hiyo ambayo inafungamna na Idara ya Masuala ya Qur'ani katika Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Kuwait amesema usajidi wa mafunzo hayo tayari umeshaanza.
Amesema wameunda makundi mapya kes mujibu wa huduma za Qur'ani wanazotoa katika kituo hicho kwa lengo la kutoa mafunzo ya Qur'ani kwa lugha kama vile Kiingereza, Kurusi na Kifaransa.
Washiriki wanaweza kujifunza kusoma Qur'ani kwa pamoja au binafsi kwa njia ya intaneti.
Taasisi ya Kutoa Kutoa Mafunzo ya Qur'ani Kupitia Intaneti nchini Kuwait inasema hadi sasa imetoa mafunzo kwa washiriki walio katika nchi 25.